Utunzaji wa mazingira
Tutunze mazingira kwajili ya vizazi vyetu na hata vizazi vijavyo
Jumapili, 26 Mei 2019
Utunzaji wa vyanzo vya maji
Jumapili, 19 Mei 2019
UTUNZAJI WA MAZINGIRA
UTUNZAJIWA MAZINGIRA
Nini maana ya mazingira?
Nini maana ya mazingira?
Mazingira ni jumla ya vitu vyote vinavyo mzunguka kiumbe hai katika maisha yake kama hewa, maji, mmea.Ili kiumbe hai aweze kuishi vizuri anahitaji mazingira safi na salama. Kwa kawaida mazingira yanahitaji utunzaji wa hali ya juu ili yaweze kuwa safi na salama. Hivyo basi maisha ya viumbe hai wa kizazi kilichopo na kijachjo kinategemea uwepo wa mausiano mazuri ya utunzaji wa mazingira
Utunzaji wa mazingira ni hali au kitendo cha kuyaweka mazingira katika hali ya usafi na salama ili kadumisha maisha ya kiumbe hai. Maisha ya kiumbe hai yanahitaji uwepo wa mazingira safi na salama. Asilmia kubwa ya mazingira duniani kama vile vyanzo maji, hali ya hewa vinazaidi kuchafuliwa kwa sababu mbalimbali. Zifuatazo ni sababu zinazosababisha uchafuzi mazingira duniani : ➤ Shughuli za viwandani ambazo husababisha uchafuzi wa hali ya hewa kwa kutoa gesi mbalimbali ambazo ni chafu.
➤ Utupaji ovyo wa taka, hii husababisha takataka nyingi kusafirishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine ambazo zinaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa kama vile kipindupindu. ➤ Ukataji ovyo wa mimea,hii inasababisha hali ya ujanngwa kutokana na ukosefu wa mimea ambazo husababisha kuundwa kwa mvua
➤ Shughuli za binadamu kama vile kilimo ambacho husababisha ukataji wa miti kwa ajili ya kuendessha kilimo chao na wengi wao hufuga idadi ya mifugo katika eneo dogo.
Pamoja na hayo yote zipo njia za kuweza kukabiliana na uchafuzi wa mazingira ili kuyaweka katika hali ya usalama, zifuatazo ni baadhi ya njia hizo:
➤Kila mwananchi ajue yakuwa nijukumu lake kupanda miti na kutunza mazingira ili kuzuia mlipuko wa majanga mbalimbali
➤ Kutumia njia za kisasa za kilimo na ufugaji, hii itasaidia kupunguza mmomonyoko wa udongo pamoja na upungufu mkubwa wa misitu.
➤Sheria kali zichukuliwe kwa watu wanaokiuka matakwa ya utunzaji wa mazingira.
/
➤ kama tukifuata maelekezo tunayopewa kuhusu utunzaji wa mazingira na kuyafanyi kazi tunaweza kuyaweka mazingira yetu katika hali ya usafi na salama hii hupunguza majanga mbalimbali kama ujanwa.
sasimalimi@gmail.com
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)
Utunzaji wa vyanzo vya maji
UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI VYANZO vya maji katika maene...